KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA ATOA WIKI MOJA RUWASA KUPEWA HATI ENEO LA MRADI MAJI MAKUYU

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfley Mnzava ametoa wiki moja kwa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo kutoa hati miliki ya eneo ulipojengwa mradi wa upanuzi wa maji Makuyu Kwenda Kinyolisi na Iyogwe ulio chini ya Wakala wa maji vijijini RUWASA


Upanuzi wa mradi wa maji Makuyu kwenda Kinyolisi na Iyogwe ni mradi uliotekelezwa kupitia fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19 na umegharimu shilingi 513,050,359.33

Ametoa agizo hilo Aprili 21 wakati akizindua mradi wa upanuzi wa miundombinu ya maji katika Kijiji cha Makuyu unaolenga kuwanufaisha wananchi 6076 wa vijiji vya Kinyolisi na Iyogwe.

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Wilaya ya Gairo Mhandisi Gilbert Isac amesema mradi huo unakwenda sambamba na kauli mbiu ya kumtua mama ndoo kichwani

Mwenyekiti wa Kijiji cha Iyogwe ambaye ni mmoja wa Vijiji nufaika Richard Yeremia Kagoda, amemshukuru Serikali Kupitia RUWASA kwani awali walikuwa wanapata changamoto katika kupata maji Safi na salama huku wakitenga siku nzima kufuata maji ya visima vya kuchimba Kwa mkono.

Ujio wa Mradi huo ulikuwa kama mkombuzi kwao, waliona ni vyema kutoa eneo hilo bure kuwezesha Mradi uanze kwa wakati.



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments