Makamu Mwenyekiti UVCCM Taifa Ndg. Rehema Sombi Omary (MNEC) amekabidhi Mizinga 10 ya kufugia nyuki kwa Umoja wa Viana wa Cham cha Mapinduzi Wilaya ya Singida mjini kwaajili ya kuanzisha mradi wa ufugaji nyuki kama kitega uchumi cha Jumuiya ya Vijana Wilayani hapo.
Ndugu Rehema Sombi amewahimiza Vijana hao kutumia mizinga hiyo kwaajili ya Kukuzia mtaji ili kuweza kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wengine.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari mwenge kwenye Kongamano la Vijana wa CCM wilaya ya Singida mjini
0 Comments