MERIDIANBET YAPIGA HODI MTAANI KUWASHIKA MKONO WAPAMBANAJI

MITAA iliitika mitaa ikaukubali mziki wa Magwiji wa Odds kubwa, Nyumba ya Mabingwa wa michezo ya ubashiri na kasino ya mtandaoni, ufalme wa washindi Meridianbet pale walipopita mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam na kuwashika mkono wapambanaji wote.

Watu wengi walijitokeza kuona ni nini Meridianbet wamewaletea na hapo ndipo tabasamu lilipofunguka mithili ya jua la asubuhi linavyochomoza, mitaa na chocho zote za Jiji la bata na salama, liliguswa kwa kupatiwa nguo za kujikinga na mvua kwa Bodaboda na abiria wote, wafanyabiashara mbalimbali nk 

Kwa niaba ya madereva bodaboda na bajaji muwakilishi wao aliyefahamika kwa jina moja la Athuman alisema “Meridianbet hakika ni mwanga wa kila mtu na leo kila mtu anafaidika na msaada huu”

Meridianbet imetoa msaada wa nguo za kujikinga na mvua kwa madereva Bodaboda na Bajaji, wafanyabiashara wa sokoni ikiwa ni sehemu ya kupambana na madhara yatokanayo na mvua zinazoendelea kunyesha katika Jiji hili la Dar Es Salaam. Kwa upande wa muwakilishi wa Meridianbet alisema kwamba;

“Kampuni inatambua mchango wa madereva hao, na hivyo wameamua kuunga juhudi zao kwa kutoa msaada wa nguo hizo ili kutoathiri kazi yao kipindi mvua inaponyesha, pamoja na madhara ya kiafya yatokanayo na kunyeshewa na mvua”

Meridianbet ni kampuni inayofanya shughuli za ubashiri mitandaoni, na michezo ya kasino ya mtandaoni, kila siku washindi wengi wanajizolea mamilioni na kutajirika, pamoja na yote hurudisha kwa jamii kile wanachokipata.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments