RAIS SAMIA NI MFUASI WA HAYATI BABA WA TAIFA MWL. NYERERE - BALOZI DKT. NCHIMBI

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa CCM ndugu. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Nkasi mkoani Rukwa.

Balozi Dkt. Nchimbi ameeleza namna Rais Samia alivyo na uzalendo wa kuwajali wananchi wake anaowaongoza na Taifa kwa ujumla ambapo amesena kuwa katika fedha za Covid - 19 zilizotolewa kwa mataifa mengi ya Afrika, wengi wao wamegawana fedha hizo wao na familia zao, ndugu zao na marafiki zao lakini kwa Rais Samia imekuwa tofauti kwakuwa ameonesha uzalendo wa kweli na dhamira yake ya dhati kwa kuelekeza fedha hizo kutumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Afya na Elimu.

"Nchi nyingi za Afrika zilizopewa fedha za Covid - 19 waligawana viongozi lakini Rais wetu Dkt. Samia alizielekeza katika maendeleo mikoani na wilayani hakuna fedha iliyobaki ikulu hata senti moja". Amesema Balozi Nchimbi.

Amesema kuwa tuna Rais Mwanadiplomasia anawaacha watu wanaongea wanachojisikia, lakini  ukipata uhuru wa kuongea basi unapata na uhuru wa kuwaza basi muwaze kwamba si sawa kumkebehi, kumsema kwa uongo na kumtukana .''Rais Samia angekuwa mbabe mngeona shida kwelikweli"

Aidha, Balozi Dkt. Nchimbi amesema CCM itatumka nguvu zake na maarifa katika kuhakikisha serikali zote zinafanya kazi wakati wote kwa kujielekeza kuleta maendeleo ya wananchi na kusiistiza kuwa Chama hakitasita kuzikosoa na kuzielekeza.










TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments