SERIKALI KUTANGAZA RIPOTI YA SENSA YA WANYAMA NA UTALII KESHO

 


Na John Mapepele
Kesho Serikali inakusudia kutangaza rasmi matokeo ya Sensa ya Wanyamapori na kuzindua taarifa ya Watalii wa Kimataifa walioitembelea Tanzania mwaka 2023 katika mkutano unaojumuisha wadau wa uhifadhi na utalii, utakaofanyika hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha.

Mkutano huo umeratibiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, ambapo Waziri mwenye dhamana na Wizara hiyo, Mhe.Angellah Kairuki anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi atakayetangaza taarifa hizo katika tukio hilo la kihistoria ambalo limepewa jina ya “kubwa mbili za Maliasili na Utalii”.
Akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari jijini Arusha leo Aprili 21, 2024 katika Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Mwakilishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Edward Kohi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo amesema taarifa hizo ni muhimu kwa katika kuboresh uhifadhi wa wanyamapori na kukuza utalii nchini na kwamba zinaakisi juhudi za Serikali kuhifadhi utajiri wa Maliasili.

“Napenda kusisitiza kuwa kesho inakwenda kuwa siku ya kihistoria kwenye taifa letu ambapo Mhe. Waziri wetu Kairuki anakwenda kuitangazia dunia mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya uhifadhi na sekta ya utalii hususan baada ya yeye mwenyewe kucheza Filamu ya Royal Tour”. Amefafanua DK. Kohi

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Wakurugenzi kadhaa wa Sekta za Wanyamapori, Utalii na Wakurugenzi kutoka TAWIRI.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments