Singida Yalipa Mamilioni Ya Fedha Kwa Stakabadhi Bandia

Halmshauri ya Singida mkoani Singida yatumia malipo ya sh. Milioni 147.29 yaliyodhibitishwa na Stakabadhi Bandia 'Fake'

Kwa Mujibu wa Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) CPA Charles Kichere pya Mwaka wa Fedha 2023/2023 ilisema kuwa katika ukaguzi alibaini kwa malipo yenye thamani ya Sh. milioni 147.29 yaliyothibitishwa na stakabadhi bandia za kielekitroni katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

Katika Ripoti hiyo hiyo CAG amependekeza OR-TAMISEMI ishirikiane na Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato (TRA) kuhuisha mfumo wa ulipaji serikalini (MUSE) na mfumo wa kodi, ambapo taasisi za umma zitaweza kujiridhisha na taarifa za kikodi za wazabuni na watoahuduma mbalimbali

waliosajiliwa na TRA pamoja na kuthibitisha usahihi wa makato ya kodi kabla ya kuidhinisha malipo yao.

Pia CAG ameshauri katika ripoti hiyo TRA kuongeza ufuatiliaji wa kubaini wafanyabiashara wasio waaminifu ambao hawatoi stakabadhi za kielekitroni na kuwachukulia hatua stahiki kwa mujibu.

Ripoti hiyo Halmashauri hiyo imetumia fedha hiyo malipo hewa ambayo ya kufanyika kwa vielelezo bandia

Na Chalila Kibuda,Michuzi Blog

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments