TANZANIA YACHAGULIWA KUWA MAKAMU MWENYEKITI BARAZA LA MAWAZIRI WA MAJI KAMISHENI YA BONDE LA MTO ZAMBEZI

TANZANIA imechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa ZAMCOM katika mwaka 2024-2025 kwenye Mkutano wa 11 wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi (Zambezi Watercourse Commission - (ZAMCOM) unaoendelea mjiji Tete Nchini Msumbiji.Uchaguzi huo umefanyika kufuatia Msumbiji kumaliza muda wake na kukabidhi uenyekiti kwa Namibia, Hivyo, Tanzania inategemewa kuwa Mwenyekiti wa ZAMCOM.

Katika mkutano huo, Tanzania imewakilishwa na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew.

Licha ya kushiriki Mkutano wa 11 wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi (Zambezi Watercourse Commission - ZAMCOM), Tanzania imefanya mazungumzo na wadau wa maendeleo na kuwakaribisha kuwekeza katika Sekta ya Maji nchini Tanzania.

Mhandisi Kundo ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo amekutana na kufanya mazungumo na Mwakilishi wa Shirika la Sweden, SwedFund.

Katika mazungumzo hayo, Tanzania imeikaribisha Taasisi ya SwedFund nchini ili kushirikiana katika maeneo ya maandalizi ya miradi ya miundombinu yenye ukubwa wa kati na wa juu.

Nae mwakilishi wa SwedFund ameahidi kushirikiana na Tanzania katika kufanya majadiliano kuhusu kuandaa miradi mahsusi.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments