''WANANCHI JIEPUSHENI NA MADALALI WA KISIASA'' Omary Kinyeto

Diwani wa Kata ya KINDAI Manispaa ya Singida OMARY KINYETO amewataka wananchi wa Kataa hiyo kujiepusha na Madalali wa Kisiasa ambao wanawarubuni wananchi kwa kuwachafua viongozi waliopo ili wasiwachague katika chaguzi zinazokuja za Serikali za Mitaa Mwaka huu na Serikali Kuu 2025.

KINYETO alisema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata hiyo ya KINDAI katika mkutano wa hadhara, akieleza Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Kata hiyo.
Alisema endapo wakirubuniwa na madalali hao itasababisha kuchagua viongozi ambao hawawezi kutatua changamoto kwa kipindi cha Miaka mitano.

Aidha alisema ni muhimu kwa wananchi kuchagua Viongozi ambao watasaidia kuleta maendeleo katika  jamii na sio kuchangua Viongozi ambao wanajali maslahi yao binafsi.
KINYETO pia ameishukuru serikali kwa kuendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi kwa kutekeleza Miradi ya maendeleo ambayo inasaidia wananchi kupata huduma za kijamii katika maeneo yao.

Katika suala la barabara alisema serikali inaendelea kutenga fedha za kujenga na kukarabati barabara za Kata hiyo ili ziweze kupitika kwa muda wote.

KINYETO alisema endapo barabara zitaweza kupitika kwa muda wote itarahisisha usafirishaji wa bidhaa na wananchi kuweza kufuta huduma za kijamii ikiwemo Afya kwa urahisi.
Aidha alisema katika Kata hiyo serikali inatarajia kujenga Barabara kwa kiwango cha Lami na hivyo wananchi waendelee kutoa ushirikiano pale wanapotakiwa kutoa ushirikiano.

Pia katika suala la Elimu, Diwani KINYETO alisema Serekali imetoa Fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha Miundombinu ya Elimu kwa kujenga Madarasa katika Shule ambazo zilikuwa na upungufu wa Madarasa katika Kata ya KINDAI.

Kutokana na Miundombinu hiyo kuboresha, aliwataka Wazazi na Walezi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kupata Elimu, kwani ni Haki yao ya msingi kupata Elimu.
Hata hivyo Diwani KINYETO ametoa Viti 207 na Sahani 660 Kataa nzima ya KINDAI kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za Kijamii pale zinapojitokeza ili wananchi kuepuka gharama za kukodi Viti na Sahani.

 Matukio Mbali Mbali Ya Picha Katika Mkutano Huo





















TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments