Waziri wa Fedha, ambae ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Dk. Mwigulu Nchemba ameendelea kuwaomba wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa sababu ameendelea kuwajali wananchi wake kila eneo kuna miradi inayogusa wananchi.
Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu alizungumza akiwa katika ziara Jimboni kwake wakati akiongea na wananchi wa kata ya Old Kiomboi wilayani Iramba mkoani Singida.
Ameeleza Rais Dk. Samia ameendelea kujenga miundombinu ya barabara na shule mpya za msingi na sekondari nchini.
Akizungumzia kuhusu elimu, Dk. Mwigulu amesema katika uongozi wa Rais huyo, amefanya makubwa katika wilaya hiyo ikiwemo kuwezesha shule mbili za kidato cha tano na sita ambapo mwaka huu zitaanza kupokea wanafunzi.
Aidha, amebainisha kuwa shule hizo ni Shelui na Ndago sekondari huku akiahidi kukamilisha shule ya ufundi.
0 Comments