Afisa Mhifadhi Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania -TAWA Kanda ya Kati WINNIE KWEKA amesema Wanyama Pori wana faida kubwa nchini kwani wanachangia 23% ya Pato la Taifa pamoja na Fedha za Kigeni kupitia Utalii.
KWEKA alisema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Manyoni katika Mkutano wa Hadhara, ambapo alisema wanyama pori ni muhimu sana kwani Taifa linapata fedha nyingi za kigeni kupitia Sekta ya Utalii.
Alisema asilimia 23 ya mapato yote nchini yanatokana na Utalii ambao unachagizwa na uwepo wa Wanyama Pori waliopo katika maeneo mbalimbali nchini.
KWEKA alisema kuwa uwepo wa Wanyama Pori katika maeneo ya Manyoni mkoani Singida ni faida kubwa kwani kuna Fedha zinazotokana na Utalii zinarudishwa kutekeleza Miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jamii.
Aidha KWEKA aliongeza kuwa fedha hizo zinazotokana na Utali zimekuwa zikiboresha na kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo katika sekta ya Afya, Elimu na Barabara na kurahisisha upatikanaji wa huduma za Jamii.
Hata hivyo amewataka wananchi kuendelea kuwalinda na kuwatunza wanayama pori waliopo nchini ili waendelee kuleta faida kwa Taifa kwani wanasaidia kutatua na kupunguza changamoto zilizopo katika Jamii kupitia fedha zinazotokana na utalii.
0 Comments