Watendaji Wa Vijiji Wametakiwa Kuhakikisha Fedha Zinazotolewa Na Serikali Kupitia Mfuko wa TASAF Zinapelekwa kwa Walengwa

                                      

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida BERTHA NAKOMOLWA amewataka Watendaji na viongozi wa Vijiji kuzisimamia kikamilifu Fedha zinazotolewa na Serikali kupitia Mfuko wa TASAF zinapelekwa kwa walengwa waliokusudiwa ili ziweze kutumika kama ilivyokusudiwa.


NAKOMOLWA alisema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Kata ya NTONGE Wilaya Singida Vijijini, akiwa katika Ziara ya Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya hiyo na maadhimisho ya Wiki ya Wazizi.

Alisema kumekuwa na changamoto ya fedha zinazotolewa na serikali kupitia mfuko wa TASAF kutowafikia walengwa wa mfuko huo, kutokana na usimamizi mbovu wa baadhi ya watendaji na viongozi wa vijiji.

NAKOMOLWA alisema kutokana na usimamizi huo mbovu kumesababisha watu ambao sio walengwa kuingizwa kwenye mpango huo wa TASAF na Kaya Maskini.

Aidha aliwataka wananchi kutoa taarifa kwenye ngazi husiki pale wanapoona kuna watu ambao hawana sifa za kuingizwa kwenye mpango huo wa TASAF wameingizwa na wananufaika kinyume na taratibu.

Alisema serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inatoa fedha nyingi kwa ajili ya kutoa Ruzuku kwa kaya masikini ili ziweze kujikimu na kuinuka kiuchumi, lakini baadhi ya viongozi wa Vijiji wanakwamisha malengo ya Rais Dkt Samia.

Nao baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida waliwataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wanakwenda shule ili waweze kupata haki yao ya msingi ya kupata Elimu.

Wajumbe hao walisema kuna baadhi ya wazazi wanawazuia watoto wao kwenda shule na kuwatumia kufanya kazi mbalimbali za nyumbani, na kuwafanya watoto hao wasiende shule.

Hata hivyo Wajumbe hao pia walitoa wananchi kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu na uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika mwaka 2025.















TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments