Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshiriki dua ya kumuombea Hayati Sheikh Abeid Amani Karume iliyofanyika katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar. Dua hiyo pia ilihudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla.
Viongozi wengine walioshiriki ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi-Bara Abdulrahman Kinana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dkt. Emmanuel Nchimbi
0 Comments