WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameitaka Timu ya mpira wa miguu ya FGA ya mkoani Ruvuma ambayo inashiriki Ligi Daraja la kwanza katika msimu huu wa mwaka 2023/24 iendelee kupambana na kufanya vizuri ili kucheza ligi hiyo msimu ujao.
Mhe.Ndumbaro ametoa kauli hiyo alipokutana na kuzungumza na timu hiyo Aprili 19, 2024 mjini Songea wakati timu hiyo ilipokua ikijiandaa kusafiri kwenda mkoani Mbeya kuikabili timu ya Mbeya City, Aprili 21, 2024.
Amewataka wachezaji wajiamini na kuonesha uwezo wao ili kuisaidia timu kusonga mbele pamoja na kuweka mazingira mazuri ya kujiuza katika soko la ndani na nje.
Aidha, Waziri Dkt. Ndumbaro amewasisitiza wachezaji hao wapambane ili kupata alama sita muhimu kwenye michezo miwili iliyobaki ambapo mchezo wao wa mwisho utakuwa dhidi ya Ken Gold ya Jijini Mbeya ili wajihakikishie kubaki katika nafasi nzuri katika ligi hiyo.
0 Comments