Serikali ya Jamhuri ya Zambia imeeleza nia yake ya kuendeleza ushirikiano nchi Jirani katika Usafirishaji wa Shehena kutoka na kuingia nchini humo, ili kukuza uchumi wa Nchi hiyo na kutumia vyema fursa zilizopo hasa katika rasilimali za Madini.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Uchukuzi na Usafirishaji wa Serikali ya Zambia Mhe. Frank Tayali wakati akifungua Kongamano la tatu Biashara na usafirishaji (Land-Linked Zambia Transport and Logistics event) Jijini Lusaka nchini Zambia
Akizungumza kando ya Kongamano hilo kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Luteni Jenerali Mathew Mkingule, amesema kongamano hilo ni muhimu katika kuitangaza Tanzania kupitia Miundombinu Wezeshi huku Mwakilishi wa TPA nchini Zambiw Hamisi Chambari akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA akisema kuwa TPA inanafasi muhimu katika kongamano hili kama Mdau muhimu katika sekta ya Uchukuzi ikihudumia nchi za SADCA ikiwemo Zambia.
TPA inashiriki kongamano hilo la siku mbili lililoanza tarehe 4 Aprili,2024 likikusisha Taasisi za sekta ya Uchukuzi kwa ukanda wa Nchi za Kusini mwa Afrika maarufu kama Zambia Land Linked Conference, kama Mdau na mmoja wa Wadhamini wakuu.
0 Comments