Africa Day Marathon kufanyika Mei 18, ni kumbukizi ya kuanzishwa kwa OAU.

 

Mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania hususani waafrika katika kukumbuka kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika (OAU) Mei 25, 1963, Adisababa Ethiopia watashiriki mbio maalumu zikilenga kumbukizi ya lengo la umoja huo katika kuzikomboa nchi ambazo hazikuwa huru.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Mashariki Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Alli Bujiku amesema mbio hizo zitakuwa za kilometa 5 na 15 na zitahusisha mabalozi na baadhi ya maofisa wa kibalozi na watanzania kwa ujumla.

Aidha amesema wanariadha wa Kitanzania ambao wameweka alama kimataifa, Juma Ikangaa, Alphonce Simbu, Filberty Bayi na wengineo wanatarajiwa kuwemo katika mbio hizo ambazo zimepewa jina la Africa Day Marathon zinazotarajiwa kufanyika Mei, 18 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Balozi Bujiku ameongeza kuwa mbio hizo maalumu ni kwa ajili ya kuadhimisha miaka 61 ya kuanzishwa OAU mwaka 1963 na mwaka 2002 kubadilishwa jina na kuitwa (AU) baada ya nchi zote za Afrika kuwa huru na sasa wakiwa wanaangalia mafanikio na kupanga mikakati ya kusonga mbele na kujiletea mafanikio katika nyanja mbalimbali.

Hata hivyo amesema nchi nyingi za Afrika zinaadhimisha siku hiyo Mei, 25 kila mwaka, ila kwa Tanzania wataadhimisha Mei 20, kutokana na Mei 25, 2024 kutakuwa na ugeni wa Baraza la Amani na Usalama.

Hata hivyo ameongeza kuwa baada ya mbio hizo, watapeleka misaada katika shule zenye wahitaji maalumu nne, mbili zikiwa za Shule za Msingi na mbili za Sekondari ambazo ni Jangwani, Pugu, Uhuru Mchanganyiko na Jeshi la Wakovu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments