ATOA ELFU TANO KWA RAIS SAMIA

 

Mkazi wa kijiji cha Luchima katika kata ya Majimoto halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile ametoa shilingi elfu tano kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi.


Kiasi hicho cha pesa kimekabidhiwa kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda tarehe 3 Mei 2024 wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Luchima alipokwenda kuzungumza nao wakati wa ziara yake ya kuwafariji wananchi waliopatwa na mafuriko katika jimbo lake la Kavuu.

‘’Nampongeza rais kwa vitendo kabisa naomba mhe, mbunge leo nikikabidhiwa fedha taslimu shilingi elfu tano umpelelekee Mhe, Rais ’’ alisema.

Kwa mujibu wa mwananchi huyo, uamuzi wake unatokana na kuwiwa na uongozi bora na utendaji kazi wa Rais Samia hasa kwa kuwajali wananchi wa Luchima ambapo mbali na mambo mengine amewajali kwa kutoa fedha milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati aliyoieleza imewakomboa wananchi wa kijiji hicho.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda amesema atahakikisha kiasi hicho cha fedha kilichotolewa na mwananchi huyo kinamfikia mhe, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Amempongeza mwananchi huyo wa kijiji cha Luchima wa uamuzi wake wa kutoa kiasi hicho cha fedha kama ishara ya kukubali juhudi na kazi kubwa inayofanywa na Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Luchima na Tanzania kwa ujumla.

Amewaaleleza wananchi wa kijiji hicho kuwa, Rais Samia anawapenda sana na amekuwa akisaidia juhudi mbalimbali za maendeleo kwenye jimbo la Kavuu na kutaja baadhi ya juhudi hizo kuwa ni pamoja na kutoa fedha za ujenzi wa hospitali, shule, barabara pamoja na upatikanaji wa huduma za maji.

Mhe, Pinda amefanya ziara katika jimbo lake la Kavuu kuwafariji wananchi waliopatwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa na kuathiri miundiombinu ikiwemo madaraja.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda akimpongeza mkazi wa kijiji cha Luchima katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile aliyetoa shilingi elfu tano kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi tarehe 2 Mei 2024.
Mkazi wa kijiji cha Luchima katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile akizungumza mara baada ya kumkabidhi shilingi elfu tano Naibu Waziri wa Ardhi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda aliyoitoa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi tarehe 3 Mei 2024.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya  Makazi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda akimpongeza mkazi wa kijiji cha Luchima katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile aliyetoa shilingi elfu tano kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi tarehe 2 Mei 2024.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments