BASHE KUONGOZA MKUTANO WA WADAU WA TASNIA YA MBEGU LEO DODOMA

Mkutano Mkuu wa wadau wa Tasnia ya mbegu  Tanzania unafanyikaleo Jijini Dodoma ambapo mgeni  rasmi ni Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe.

 Miongoni mwa mada zitakazowasilishwa kwenye mkutano huo wadau wa Tasnia ya mbegu ni Hali ya Tasnia ya mbegu na mpango wa uendelezaji mbegu, Majukumu ya SAGCOT katika kuwezrsha upatikanaji wa mbegu za mazao  ya biashara na viazimviringo na Mikakati ya kuwezrsha upatikanaji wa mbegu za awali za mazao mbalimbali.

Mada zingine ni fursa za biashara ya mbegu Bora'' za mazao ya Kilimo , uthibiti wa ubora wa mbegu,fursa za ajira za wanawake na vijana kupitia Tasnia ya mbegu, upatikanaji wa mbegu Bora'' za mazao ya mbogamboga na Miche Bora'' ya miti ya matumda na mada  ya kujengea uwezo  wazalishaji mbegu kupitia BBT.

Baada ya Majadiliano wadau hao watatoka na maazimio ya pamoja  lengo likiwa yale watakayokubaliana yatatekelezwa.

Aidha maonesho ya wadau wa mbegu yapo katika eneo la viwanja  vya Hotel ya Morena Jijini Dodoma.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments