Barrick Yapongezwa Kwa Kutekeleza Sera Ya Local Content Kwa Vitendo Na Kunufaisha Watanzania.

Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Melkiory Ngido akisalimiana na Waziri wa Madini, Antony Mavunde alipotembelea banda la Barrick akiongoza ujumbe wa viongozi mbalimbali wa Serikali.

Na Mwandishi Wetu.

Waziri wa Madini, Mh.Antony Mavunde, ameipongea kampuni ya dhahabu ya Barrick nchini kwa kutekeleza kwa vitendo sera ya ushirikishaji watanzania na kuwanufaisha kupitia mnyororo wa uwekezaji katika sekta ya madini (Local content).

Pongezi hizo zilitolewa wakati wa mkutano wa Jukwaa la tatu la utekelezaji na ushirikishaji watanzania katika sekta ya madini unaondelea katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.

Akiongea baada ya kutembelea banda la maonesho ya Barrick lililopo kwenye eneo la mkutano huo baada ya kupata maelezo jinsi kampuni inavyotekeleza sera hiyo kutoka kwa Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Melkiory Ngido, Waziri Mavunde ambaye alifungua rasmi mkutano huo amesema Barrick ni mfano wa kuigwa katika utekelezaji wa sera ya Local content kutokana na uwekezaji wake nchini kwa kwa na serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals.

Waziri Mavunde, alipongeza pia mchakato mzuri wa kufunga mgodi wa Barrick Buzwagi uliofanywa na Barrick kwa jinsi ambavyo tayari umeanza kufungua milango ya kiuchumi mkoani Shinyanga na mikoa mingine ya kanda ya ziwa na nchi jirani.

Awali akitoa maelezo kwa Waziri wa Madini aliyeongeza ujumbe wa viongozi mbalimbali wa Serikali,Meneja wa Barrick nchini,Melkiory alieleza jinsi kampuni ya Barrick inavyoendelea kunufaisha wazawa kupitia sera hii ya Local content ambapo asilimia kubwa ya manunuzi kwenye migodi yanafanyika kutoka kwa wazabuni wazawa.

Barrick imekuwa ikitekeleza sera hii kwa vitendo katika maeneo ya ajira ,utoaji wa zabuni sambamba na kufanikisha miradi ya kijamii katika maeneo yanayozunguka migodi kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR).

Barrick inayo programu ya kuwaendeleza wafanyabiashara wazawa (Local Business Development Programme) ambayo ni mhimili katika kusimamia sera hii na tayari wafanyabiashara wamekuwa wakipatiwa mafunzo katika awamu mbalimbali kupitia programu hii.


Waziri wa Madini, Mh.Antony Mavunde (wa kwanza kulia) akipata maelezo ya jinsi Barrick inavyowezesha watanzania kupitia uwekezaji wake kutoka kwa Meneja wa Barrick nchini Melkiory Ngido (kushoto) alipotembea banda la maonesho la kampuni hiyo kwenye mkutano wa Jukwaa la tatu la utekelezaji na ushirikishaji watanzania katika sekta ya madini unaondelea jijini Arusha katika ukumbi wa AICC.
Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Melkiory Ngido katika mkutano huo.


Wafanyakazi wa Barrick wanaoshiriki mkutano huo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments