HITILAFU za nyaya baharini zimesababisha kukosekana kwa huduma ya intaneti na huduma za simu za kimataifa nchini Tanzania leo kuanzia majira ya saa tano asubuhi.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Nape Nnauye kupitia ukurasa wake wa X awali Twitter, ameeleza kuwa taarifa kutoka kwa watoa huduma wa nyaya za baharini (Submarine cables,) Seacom na EASSy zimeeleza kuwa hitilafu za nyaya kati ya Msumbiji na Afrika kusini na kusababisha kukosekana kwa huduma nchini Tanzania.
Aidha Nape amewataka watanzania kuwa watulivu wakati jitihada za utatuzi wa tatizo hilo unaendelea na upatikanaji wa huduma za intaneti na huduma za simu za kimataifa utakuwa wa kiwango cha chini na njia mbadala zitatumika hadi tatizo litakapotatuliwa
0 Comments