Mbunge wa Jimbo la Singida Vijijini RAMADHAN IGHONDO amemshukuru Rais Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN kwa kuendelea kutatua changamoto za wananchi wa Jimbo hilo kwa kutekeleza Miradi mbalimbali ya maendeleo.
IGHONDO alisema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa kijiji cha msisi, wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ALLY HAPI jimboni hapo.
Alisema kwa sasa changamoto zimepungua sana kwani wananchi wanapata huduma za kijamii katika maeneo yao tofauti na zamani ambapo iliwalazimu kutembea umbali mrefu kufuata hudumu.
Aidha alisema katika sekta ya maji kwa sasa asilia kubwa ya Vijiji imefikiwa na huduma ya maji safi na Salama, hali ilisababisha wananchi kuacha kutembea umbali mrefu kufuata Maji.
IGHONDO alisema zamani akina Mama wengi walitumia muda mwingi kufata maji kwenye visima na makorogo na kusababisha kushindwa kufanya shughuli za uzalishaji mali.
Katika sekta ya miundombinu ya Barabara, IGHONDO alisema kwa sasa asilimia kubwa ya Barabara za jimbo la Singida Vijijini zinapitika tofauti na zamani ambapo ilikuwa ni shida kwa baadhi ya maeneo yalikuwa hayapitiki hasa kipindi cha masika.
Barabara zinapitika kwa nyakati zote kwa sasa na wananchi kwao imekuwa rahisi kuzifikia huduma za kijamii kama vile afya na kusafirisha mazao yao kwenda kwenye masoko.
Hata hivyo IGHONDO alisema Rais Dkt. SAMIA amejenga Vituo vya Afya kila Kata na Zahanati kila Kijiji kwa lengo la kuwaondolea adha ya kufuata huduma za Afya umbali mrefu.
Nao baadhi ya wananchi wa walisema wanashukuru serikali kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa kipindi kirefu na hivyo hawatamuangusha Rais Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu na uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika 2025.
Wananchi hao walisema watahakikisha wanakiunga mkono chama cha Mapinduzi - CCM kuchagua wagombea wa Chama hicho ili kichukue viti vyote vya uongozi na ngazi ya maamuzi.
Picha za viongozi mbali mbali waliokuepo katika mkutano huo.
0 Comments