MWANAFUNZI WA DUCE AIBUKA NA MFUMO WA KUZUIA UPOTEVU WA MAJI NA KULINDA UHARIBIFU WA PAMPUBw. Kalua Polikarpo, Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu (BSc. Ed) kutoka katika Idara ya Fizikia, Hisabati na Infomatiki ( PMI ) iliyo chini ya Kitivo cha Sayansi ( FoS ) abuni mfumo wa kudhibiti mtiririko wa maji unaotokea pindi maji yanapojaa kwenye matanki na kuzuia uharibifu wa pampu.

Hayo yamedhihirika katika Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2024 yanayoendelea hapa jijini Tanga

DUCE tunayo furaha kubwa kuujulisha Umma kuwa Bw. Kalua Polikarpo, Mwanafunzi wetu wa Mwaka wa Tatu anayesoma _Shahada ya Sayansi ( Hisabati na Fizikia) na Elimu_, ameonesha ujuzi wa hali ya juu kwa kubuni mfumo wa kuzuia upotevu wa maji na kupunguza uwezekano wa kuungua kwa pampu kutokana na kuvuta upepo kwa muda mrefu. 

Akifafanua hayo, Bw. Kalua amesema mfumo huo utasaidia kuratibu matumizi bora ya maji. 

Zaidi amesema kuwa mfumo huo mpya utaokoa gharama za matengenezo na ununuzi wa pampu mpya. 

Kimsingi, mradi huu utaleta suluhisho muhimu kutokana na changamoto zinazoikabili jamii yetu. Aidha, ubunifu huu unadhihirisha uwezo wa wanafunzi wetu katika nyanja za elimu, sayansi, na teknolojia.

 Kwa dhati, tunampongeza na tunajivunia ubunifu huu ambao ni chachu kwa maendeleo ya jamii na Taifa. 

Karibuni katika viwanja vya Popatlal jijini Tanga, kushuhudia na kujifunza zaidi kuhusu maonesho ya miradi mbalimbali yenye ubunifu wa hali ya huu kama huu kutoka kwenye Chuo chetu. Hii inadhihirisha kuwa DUCE ni zaidi ya ualimu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments