UMOJA WA WAFUGAJI NYUKI WAKUTANA KIJIJI CHA NYUKI ,KISAKI SINGIDA

Mkurugenzi wa Kijiji cha Nyuki PHILEMON KIEMI amekutana na viongozi wa wafugaji wa Nyuki kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Singida kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wafugaji wa Nyuki.

KIEMI alisema kuanzishwa kwa umoja wa wafugaji wa Nyuki Mkoa wa Singida itasaidia kutatua changamoto zinazowakabili wafugaji wa Nyuki kwa kuweka mikakati itayosaidia kupunguza au kuziondoa kabisa changamoto hizo.

Alisema Kijiji cha Nyuki kimegawa mizinga 421 kwa wananchi wa halmashauri zote za Mkoa wa Singida ambao waliokuja kupata mafunzo ya ufugaji nyuki ili waweze kufuga Nyuki kibiashara.

KIEMI aliongeza kuwa matunda ya mafunzo hayo na mizinga hiyo imeanza kuleta matokeo baada ya baadhi ya wafugaji wa Nyuki kuleta Bidha walizovuna kuja kuziuza kijiji cha Nyuki.

Baadhi ya viongozi hao wa wafugaji wa Nyuki walisema changamoto kubwa iliyopo kwa sasa ni uhaba wa mizinga kwa wananchi.

Walisema uhaba huo wa miszinga unasababisha wananchi kuendelea kufuga Nyuki kienyeji, hivyo ni vyema elimu iendelee kutolewa juu ya matumizi Bora ya Miziga ya kisasa ambayo itasaidia wafugaji wa Nyuki kuzalisha mazao mengi na bora yanayotoka na Nyuki.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments