Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ALLY HAPI amewataka Viongozi Chama cha Mapinduzi CCM na Jumiya zake kujipanga na kuweka mikakati ya kuhakikisha wanaimarisha Chama ili kushinda ngazi zote za Uongozi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
HAPI alitoa wito huo wakati akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Kintinkuu wilayani Manyoni, mkoani Singida akiwa katika Ziara yake ya kikazi mkoani hapa ya kuimarisha Jumuiya hiyo na Chama cha Mapinduzi.
Alisema ni muhimu sana kwa Jumuiya zote za Chama cha Mapinduzi na Chama kwa jumla kuhakikisha uchaguzi unapofika kusiwe na dosari yoyote itakayosababisha kupoteza baadhi ya ngazi za uongozi na badala yake ngazi zote za uongozi ziwe chini ya CCM.
HAPI pia alisema ili kuhakikisha chama kinakuwa imara na Jumuiya zake ni lazima Viongozi wa CCM wayasema mazuri yanayofanywa na Rais Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN kupitia Ilani ya CCM.
Alisema Miradi mingi imekamilika na kuwa mkombozi kwa wananchi katika kutoa huduma kwa wananchi chini ya Rais Dkt SAMIA SULUHU HASSAN, hivyo ni muhimu wananchi wakaamua hayo.
Aidha HAPI aliwataka Viongozi wa Chama cha Mapinduzi - CCM kuendelea kuhakikisha wanasima utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye ngazi zote ili kuhakikisha Miradi yote iliyobakia inakamilishwa kwa wakati.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida BERTHA NAKOMOLWA alisema Jumuiya hiyo imejipanga kikamilifu kuhakikisha ina kuwa imara mkoani hapo, kwa kuhakikisha uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchungu Mkuu wa 2025 CCM inashinda kwa kishindo.
NAKOMOLWA aliongeza kuwa Jumuiya hiyo pia itahamasisha wanawake wajitokeze kwa wingi kuchukua Fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika maeneo yao ili waweze kushiriki katika ngazi mbalimbali za maamuzi.
Alisema pia Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida inaendelea na ujenzi wa nyumba za watumishi wa Jumuiya hiyo kila Halmashauri, ambapo baadhi ya halmashauri tayari nyumba hizo zimekamilika na watumishi wameanza kuishi kwenye nyumba hizo.
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Singida waliishukuru Serikali kwa kuendelea kuleta maendeleo kwa wananchi kwa kutekeleza Miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Miradi ya Maji, Afya, Elimu na Miundombinu ya Barabara.
Walisema kupitia Miradi hiyo, upatikanaji wa huduma za kijamii umekuwa rahisi ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambacho wananchi walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata hudumu hizo za kijamii.
0 Comments