MRADI wa kuboresha Mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki (BEVAC) umewafikia wafugaji nyuki wapatao elfu 10,371 kwaajili ya kuwashika mkono katika vitu mbalimbali ikiwemo vifaa na mafunzo ambapo tayari wameshawafikia wafugaji elfu 3,200 na elfu 7000 kuwatambua na kuwakusanya.
Hayo yamebainishwa leo Mei 20,2024 na Mfuatiliaji na Tathmini kwenye mradi wa BEVAC, Deogratius Kimena kwenye Maonesho ya Siku ya Nyuki Duniani ambayo yamefanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Aidha amesema kuwa mradi huo unafanyakazi na wadau wengine ambao wapo kwenye mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki ambapo katika wadau hao ni pamoja na watoa huduma za kigani katika sekta hii kuwezeshwa, ambao hao ni Maafisa ufugaji nyuki wa Wilaya na Maafisa maliasili wa Mkoa ambao ndio wanasimamia ufugaji nyuki kwenye Mikoa.
"Mradi umeshawafikia wafugaji nyuki 10,371 kwaajili ya kuwashika mkono kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo vifaa pamoja na mafunzo,na mpaka sasa tumewafundisha wafugaji 3,200 ma tunaendelea na hao 7,000 ambao tumeshawatambua na kuwakusanya kwaajili ya kuendelea kuwapatia mafunzo". Amesema
"Mradi pia unafanyakazi na wadau wengine ambao wapo kwenye mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki katika hao wadau mradi pia unawawezesha watoa huduma za kigani katika sekta hii ya ufugaji nyuki yaani Maafisa ufugaji nyuki wa Wilaya pamoja na Maafisa Maliasili wa Mkoa ambao ndio wanasimamia ufugaji nyuki kwenye Mikoa yao kwahiyo kwa Maafisa, mradi umeweza kutoa mafunzo,vifaa,mradi pia umetoa pikipiki katika Wilaya 19 ambazo tunafanyiakazi ili waweze kuwafikia wafugaji nyuki kwa wepesi zaidi". Amesema
Aidha Kimena amesema kuwa Mradi ulipangwa kufanywa kwa miezi 54 ambapo ulianza tarehe 1/09/2021 na utaisha 28/02/2026. Na Bajeti ya ya mradi huu ilikuwa ni Euro milioni 10 sawa na Shilingi Bilioni 27 kwa wakati huo mradi ulipoanza maana thamani ya fedha huenda ikibalika kwa kupanda na kushuka.
"Mradi ulipangwa kufanywa kwa miezi 54 na mradi ulianza tarehe 1/09/2021 na utaisha tarehe 28/02/2026,hivyo mradi utaenda kwa miaka 4". Bajeti ya mradi huu ilikuwa ni jumla ya Euro milioni 10 ambazo ni sawa na Bilioni 27 thamani hii ilikuwa ni kwa mradi ulipoanza maana thamani ya fedha hupanda na kushuka". Ameongeza.
Sambamba na hayo pia ameitaja mikoa mi 5 kwa Tanzania Bara na miwili kwa Pemba ambayo inatekeleza mradi huu wa BEVAC ikiwa ni pamoja na Kigoma,Katavi,Singida, Tabora na Shinyanga,kwa Pemba ni Pemba kaskazini na Pemba Kusini na kwa yote hiyo wanafanya katika Wilaya 19 na si Wilaya zote za Mikoa hiyo.
"Mradi unatekelezwa kwenye Mikoa 5 Tanzania Bara na kisiwani Pemba kwahiyo kwa jumla ni Mikoa 7 kwasababu Pemba kuna mikoa 2 ya Pemba kaskazini na Kusini, Tanzania Bara ni Kigoma,Katavi, Tabora,Singida na Shinyanga lakini katika hiyo mikoa tunafanya kazi kwenye Wilaya 19 kwamaana hiyo sio Wilaya zote za hiyo mikoa ,Tumeangalia yale maeneo yenye uzalishaji wa juu wa mazao ya nyuki na ambayo uwezo wa uzalishaji uko chini kwa vifaa na rasilimali na tunawajengea uwezo pia".
"Mradi huu pia haujajifunga tunafanyakazi na wadau wote. Kwenye upande wa masoko tunafa ya na wafanyabiashara wengine ambao wako nje ya Mikoa hii ya mradi,tunafanya hivyo kwasababu mfanyabiashara anaweza kuwa Mkoa mwingine mfano Dar es Salaam lakini mzigo na mazao anachukulia Mkoa mwingine ambao unazalisha asali mfano Tabora ndo maana hatujachagua wafanyabiashaea kutoka maeneo hayo ya mradi". Ameeleza
Naye mmoja wa wanufaika wa mradi huu wa BEVAC Bi. Amina Hassan Madeleka ambaye ni Mkurugenzi wa Mwangaza Honey and food processing na Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara Mkoa wa Tabora (TWCC) na mwanamke mfugaji nyuki amesema kuwa mradi wa BEVAC umewasaidia sana katika kuwafundisha mbinu mbalimbali za kiushindani katika masoko kama vile kuwa na lebo ya bidhaa,Vifungashio vya kisasa ambavyo hapo awali hawakuwa navyo lakini pia suala la huduma kwa wateja imewafanya kuwa watofauti sana tofauti na hapo awali kabla hawajaingia katika mradi huu.
"Mradi huu kabla haujaja nilikuwa sielewi namna ya kutunza kumbukumbu, jinsi ya kujitangaza katika mitandao ya kijamii ili kupata masoko na namna ya kuyafikia masoko,jinsi ya kutengeneza leo za bidhaa zangu ili ninapoingia katika ushindani wa masoko niwe tofauti ".
"Sasa baada ya kuja mradi ndo nimeyapata haya yote,nadhani hata ukipiga picha katika meza yangu utaina iko tofauti na wengine. Mimi kutofanana na wengine ni kutokana na kupata mafunzo kutoka BEVAC mafunzo ya lebo na vifungashio kwani vinaita wateja".
"BEVAC walitufundisha mbinu za ushindani kwenye masoko kwa lebo,vifungashio na huduma kwa wateja unapokuwa kwenye biashara hivyo walitufundisha kujisimamia ili hata mradi utakapoisha tubakj tumesimama na ndio maana wametuleta kwenye maonesho kujifunza ili tudumu kuwa tofauti na wengine".
Aidha Amina ameongeza kuwa BEVAC imempigisha hatua lakini pia imemsaidia kukuza mtandao wa biashara kwa kutoka kwenda kwenye mafunzo maeneo mbalimbali kwa kukutana na watu na kubadilisha uzoefu.
"BEVAC imeweza kunipigisha hatua lakini pia imeniunganisha na watu,kwsababu tunapokutana kwenye mafunzo maeneo tofauti tofauti tunabasilishana uzoefu a kupata mtandao wa biashara ".
Mradi huu umefadhiliwa na umoja wa ulaya,unatekelezwa na Shirika la Maendeleo la Ubelgiji kwa kushirikiana na kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC) lakini ikiwa chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii na ndio inayosimamia katika utekelezaji wa mradi huu.
0 Comments