AKHSANTE FOUNDATION WACHINJA NA KUGAWA NYAMA YA NG'OMBE, KONDOO NA MBUZI MIRERANI

TAASISI ya Akhsante Foundation Tanzania imechinja ng'ombe 350, kondoo na mbuzi 1,800 za nyama na kugawa kwa yatima, wajane, wahitaji na taasisi mbalimbali za mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid El Adha.

Nyama hizo zimechinjwa kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid El Adha mji mdogo wa Mirerani na kusimamia na taasisi ya kijamii ya Akhsante Foundation Tanzania ambayo inaendesha shughuli zake sehemu mbalimbali za Tanzania bara.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo Katada Hashimu Kimaro amesema wamechinja ng'ombe 350 kondoo na mbuzi 1,800 na kugawa nyama hizo kwa wahitaji.

Kimaro amesema lengo ni kuhakikisha wahitaji wanapatiwa msaada huo ili waweze kusherehekea sikukuu ya Eid El Adha kwa furaha na amani.

"Tunatarajia kukamilisha shughuli hiii kwa muda wa siku mbili kwa kuhakikisha walengwa wote wanapata nyama hizo kwa ajili ya kusherehekea sikukuu hii ya Idd," amesema Kimaro.

Amesema wajane, yatima, vituo vya watoto wenye uhitaji na taasisi mbalimbali za eneo hilo zimegawiwa nyama hizo kwa ajili ya kusherehekea sikukuu hiyo.

Mmoja kati ya wakazi wa mji mdogo wa Mirerani, Asia Juma amesema amesherehekea sikukuu hiyo kwa kupatiwa nyama ya mbuzi atakayotumia na watoto wake.

"Sisi wajane tumeshukuru kwa kupatiwa msaada huu ambao kwa namna moja au nyingine utatusaidia katika kusherehekea sikukuu hii," amesema.TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments