MCHUNGAJI PETER MSIGWA AJIUNGA NA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

                  

Mchungaji Peter Msigwa amejiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na amepokelewa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM NEC kinachoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Daktari Samia Suluhu Hassan

Alizaliwa Juni 8 1965, ni mwanasiasa Mtanzania aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Iringa Mjini (2015-2020)

Kwa sasa Mchungaji Msigwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

Hivi karibuni 30 Mei 2024 Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Sugu, alimshinda Mchungaji Peter Msigwa kwenye Cheo cha Uwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa.

Katika uchaguzi wa kanda hiyo uliofanyika ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Makambako, ambao ulikuwa na mchuano mkali, Sugu aliibuka kidedea baada ya kupata kura 52 sawa na asilimia 51 dhidi ya Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aliyepata kura 51 (asilimia 49). Matokeo hayo Mchungaji Msigwa hakukubaliana nayo kwa kile alichodai haki haikutendeka na alikata rufaa

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments