MSD SHIRIKIANENI NA WABUNGE KATIKA USAMBAZAJI WA VIFAA TIBA KWENYE MAJIMBO.

Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) kushirikiana na Wabunge kusambaza vifaa tiba ikiwemo vitanda vya kujifungulia katika majimbo yote 214 ya Tanzania Bara.


Waziri Ummy ametoa maelekezo hayo kwa MSD leo Juni 10, 2024 Bungeni Jijini Dodoma mara baada ya kujibu maswali ya Wabunge ambapo pia Mwenyekiti wa Bunge Dkt. Joseph Mhagama alihoji juu ya changamoto ya utekelezaji wa maagizo na maelekezo ya Viongozi wa Serikali kupitia watendaji.

“Katika mwaka wa fedha huu ambao tunakaribia kuumaliza, tumesambaza vitanda vya kujifungulia katika majimbo yote 214 ya Tanzania Bara, nilitoa maelekezo kwa MSD kuwa vitanda hivi vikakabidhiwe kwa Wabunge ili wao waweze kuvipeleka katika Hospitali na Vituo mbalimbali” amefafanua Waziri Ummy Mwalimu.

"Haya ni maelekezo ya Serikali yazingatiwe na sio tu vitanda vya kujifungulia ni pamoja na vitu vilivyonunuliwa na Serikali ikiwemo magodoro, Mashine za Ultrasound pamoja na X-Ray” amesisitiza Waziri Ummy.

Amesema kuwa Serikali inawajibika kwa wananchi kupitia kwa Wabunge hivyo ni lazima tuhakikishe ushiriki wa Wabunge katika masuala mbalimbali ya miradi inayotekelezwa na Serikali katika Sekta ya Afya.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments