NAIBU WAZIRI MKUU, DK BITEKO KUFUNGUA MAONESHO WIKI YA NISHATI JADIDIFU DAR ES SALAAM


Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA), kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati kwa udhamani mkuu wa SUN KING, inawaalika Wananchi wote katika Maonesho ya Kitaifa ya Nishati Jadidifu (Renewable Energy)  yatakayofunguliwa Alhamisi Juni 6 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri Nishati, Dk Doto Biteko na kufungwa na Waziri wa Kilimo, Husein Bashe Ijumaa, Juni 7, mwaka huu. 

Kaulimbiu ya Mwaka huu ni: NISHATI JADIDIFU KWA UCHUMI SHIRIKISHI NA WA KIJANI (RENEWABLE ENERGY FOR INCLUSIVE AND GREEN ECONOMY)

Wiki ya Nishati Jadidifu itakuwa na maonesho yanayohusisha Umeme wa Jua yaani Sola, Upepo, Joto-ardhi na majiko banifu sambamba na warsha yenye mada mbalimbali kuhusu nishati jadidifu. 

Wadau wa maendeleo, kampuni na taasisi binafsi na serikari watakuwa katika mabanda kutoa elimu na kuuza bidhaa mbalimbali za nishati jadidifu kutoka kwa wataalamu waliobebea.

Wadhamini wengine wa Maonesho hayo yatakayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Posta, Dar es Salaam ni Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU), Expertise France, Ensol, GOGLA, Tanesco, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), AECF na UNDP

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments