Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego ameendelea kusikiliza na kutatua kero za wananchi ikiwa ni mwendelezo wa kampeni aliyoizindua hivi karibuni.
Dendego ameendesha kampeni hiyo, baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kidarafa Kata ya Mwanga wilayani Mkalama mkoani Singida.
Amesema amedhamiria kwa dhati kuhakikisha wananchi wanaondokana na kero kwa lengo la kuwaacha salama wakiendelea na shughuli za uzalishaji mali unaoendelea kuwepo kutokana na utulivu aliouweka Rais Dk. Samia Suluhu nchini.
Dendego katika kampeni hiyo ameambatana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Martha Mlata, Katibu wa Chama hicho, Lucy Shee, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa mkoa huo, Elphas Lwanji Mkuu wa Wilaya hiyo, Moses Machali na viongozi wengine.
0 Comments