Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake UWT Mkoa wa Singida MARTHA KAYAGA amewataka amewataka wananchi kuwatumia Viongozi waliopo katika maeneo yao kutatua Kero na Changamoto zao zinazowakabili kwani viongozi hao ndio wawakilishi wa Rais katika maeneo yao.
KAYAGA alisema hayo wakati wakizungumza na wananchi na wanachama wa CCM wa Manispaa ya Singida akiwa katika Ziara ya Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wanawake UWT Mkoa wa Singida ya kuimarisha Jumuiya hiyo, Kuandisha Wananchama Wapya na kuwaandaa wananchi kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Alisema Viongozi waliopo katika maeneo yao wanamuwakilisha Rais Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN katika kutatua changamoto za wananchi, hivyo wananchi wawatumie viongozi hao kutatua Kero na Changamoto zilizopo.
KAYAGA pia aliongeza kuwa viongozi wa serikali za vijiji na watendaji wahakikishe wanawasikiliza wananchi wanapopelekewa changamoto na kuzitatua pale inapowezekana.
Katika kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu KAYAGA aliwataka watakaohusika na utoaji wa Fomu wakati wa uchaguzi wa serikali za Mitaa kutoa Fomu hizo kwa Haki.
Alisema kuna baadhi ya watu wanahusika na utoaji wa Fomu hizo kuficha Fomu na wakati mwingine kuzitoa kwa upendeleo bila kuangalia kama wananchi hao wanaotaka kuchukua Fomu wana vigezo na sifa za kugombea nafasi mbalimbali zitakazotangazwa.
Nao baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT Mkoa wa Singida waliwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Mbaraza UWT Taifa Mkoa wa Singida JOICE MKOMA aliwataka wananchi hasa wanawake wenye sifa na vigezo kujitokeza kwa wingi kuchukua Fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Hata hivyo MKOMA alitoa wito kwa wanaume kuwaunga mkono na moyo wanaweke watakaojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
0 Comments