WANAWAKE WAMETAKIWA KUSIMAMA IMARA KUMTETEA RAIS DR. SAMIA NA KUACHANA NA WATU WANAOMSEMA KWA UBAYA

                             

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake (UWT) Mkoa wa Singida MARTHA KAYAGA amewataka Wanawake kusimama imara  na Rais Dkt SAMIA SULUHU HASSAN na kuachana na watu wanaomsema kwa ubaya na kutaka kuligawa Taifa kwa kuvuruga amani iliyopo nchini.


KAYAGA alisema hayo Wilayani Iramba, wakati akizungumza na Wananchi, ambapo aliwataka Wanawake kusimama imara kumtetea Rais Dkt SAMIA SULUHU HASSAN, kwa kutowasikiliza watu wanaomsema vibaya na kutaka kuligawa Taifa.
                                     

Alisema kuna baadhi ya wanasiasa wanapita pita na kumsema vibaya Rais Dkt SAMIA, wakati Rais ametekeleza miradi mingi ya maendeleo na kuwatatulia wananchi kero na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao.

KAYAGA pia aliwataka wananchi kuendelea kumuamini Rais Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN na Serikali yake katika utekelezaji wa Miradi mbalimbali ambayo inaendelea kutatua changamoto zinazowakali katika maeneo yao.

Katika hatua nyingine KAYAGA aliwataka  Wazazi na Walezi wanaozuia watoto wao kwenda Shule kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

Alisema Serikali imejenga miundombinu mizuri ya shule za Msingi na sekondari ili kuweka mazingira mazuri ya kujifunza na kufundishia, hivyo hakuna sababu ya Mzazi au malezi kumzuia mtoto kwenda shule.

Nao baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo ya UWT wakatoa salamu zao kwa Wananchi.

Kwa upande wake Mbaraza UWT Taifa Mkoa wa SingidaJOICE MKOMA aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt SAMIA SULUHU HASSAN kwa kuendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

                                    
JOICE pia alitoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kuchukua Fomu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu ili kuwa na viongozi wengi wanawake watakaoshiriki katika ngazi mbalimbali za maamuzi.

Hivyo aliwataka Wanawake kuacha uoga wa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi huo wa serikali za Mitaa.
                          
Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wanawake - UWT Mkoa wa Singida inafanya ziara katika Halmashauri zote za Mkoa wa Singida ya kuimarisha Chama na Jumuiya hiyo, na kutoa elimu kwa wananchi kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments