Awali akitoa taarifa fupi kwa Mgeni rasmi juu ya Mashindano hayo Afisa Michezo Mkoa Kagera Bw Keffa Elias amesema kuwa Mashindano hayo yalianza rasimi tarehe 25 May Mwaka huu na mpaka sasa hawajapata changamoto za kukwamisha Mashindano hayo.
Amesema jumla ya washiriki katika mashindano hayo walikuwa 849 huku wana michezo (wanafunzi) wakiwa 744 walimu pamoja na wasimamizi 105 na kuongeza kuwa baada ya mashindano hayo kimkoa kuhailishwa ni kuandaa timu itakayouwakilisa Mkoa pia kujipanga kwa mashindano mengine ya 2025.
Kwa sasa tunazo timu 8 kwa maana ya kila Halmshauri na timu yake ila baada ya kuhailisha leo ndugu mgeni rasmi tutaunda timu moja ambayo itaenda kushindana kitaifa ili kuuwakilisha Mkoa wetu wa Kagera,amesema Keffa".
Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo Afisa elimu Msingi wilaya ya karagwe Bw Alloys Maira aliyehudhuria kwa niaba ya Afisa elimu Mkoa amesema kuwa michezo kwa wanafunzi inayo faida kubwa ikiwemo kujikinga na magonjwa nyemelezi huku akiwasisitiza wanafunzi pamoja na walimu kuzingatia suala la michezo ili kukuza na kutambua vipaji vya watoto.
"Niwambie watoto wangu Mungu amempa kila mmoja kipaji chake hivyo kama umejaaliwa kuimba imba,kuruka ruka kucheza mpira cheza tu huwezi kujua wapi utatokea naomba mniahidi leo ni wangapi wakitoka hapa watafuatilia michezo amesema Maira"
Pia Maira amewasisitiza wale watakaobaki kambini kwa ajili ya maandalizi ya kuuwakilisha mkoa ,kuwa kwenda ngazi ya taifa sio lele mama hivyo wanabidi kupambana na kuvuna walichokipanda .
Nao baadhi ya wanafunzi kutoka wilaya Biharamlo wameshukuru kwa hatua hiyo ya ushindi na kuahidi kuweka bidii zaidi katika ngazi inayofuata pia nayo timu kutoka wilaya ya Ngara imehaidi kuongeza juhudi zaidi katika mashindano yajayo .
0 Comments