Gwiji wa Brazil Zico aporwa Ufaransa

GWIJI wa soka wa Brazil Arthur Antunes Coimbra maarufu Zico amekuwa muathirika wa wizi katika Michezo ya Olimpiki Paris 2024 baada ya mkoba wake wenye fedha na vito vyenye thamani ya jumla ya pauni 420,000 kuibiwa.

Licha ya ulinzi mkali uliopo katika michezo hiyo Zico ameibiwa vitu hivyo vya anasa wakati akisafiri kwenye gari la kukodi.

Sherehe za ufunguzi wa Michezo ya 33 ya Olimpiki katika uwanja wa mnara wa Eiffel jijini Paris Julai 25, 2024.

Ripoti zimesema Zico mwenye umri wa miaka 71 amekwenda Ufaransa kutazama Michezo ya 33 ya Olimpiki iliyofunguliwa Julai 26 na sasa amekumbwa na wizi huo ambao umemfanya kupata hasara kubwa ya kifedha.

SOMA: Wahuni wachoma moto mifumo ya treni Ufaransa

Zico aliondoka kwenye hoteli aliyofikia jijini Paris na alikuwa akisafiri akiwa na mkoba wenye mkufu wa almasi, fedha taslimu na saa ya mkononi aina ya Rolex ya gharama kubwa.

Kwa mujibu wa ripoti ilikuwa ni kipindi hicho cha safari kwa gari la kukodi ndipo watu wawili walipolikaribia gari, mmoja akizungumza na dereva wakati mwingine akielekea nyuma ya gari.

Kisha mkoba wa Zico uliporwa na watu hao wawili kukimbia.

Watalii wanaokwenda Paris kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki wamekumbushwa kuwa makini wanaposafiri kuzunguka jiji hilo.(Picha: MailOnline)

Polisi wa Paris wameanza uchugnuzi wa tukio hilo na Brigedi ya Ufaransa ya Kudhibiti Ujambazi inataraajiwa kusimamia kuwapata wahalifu.

Wanamichezo 10,714 wanatarajiwa kushiriki katika matukio 329 ya michezo 32 Tanzania ikiwakilishwa na wanamichezo 15.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments