Mawaziri wa Utalii Afrika Wakutana Zambia

ZAMBIA:  Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism), Zurab Pololikashvili amezitaka nchi za Afrika kushirikiana katika utekelezaji wa miradi ya utalii na kutafuta  fursa mbalimbali za uwekezaji katika Sekta ya Utalii.

Pololikashvili ameyasema hayo katika mkutano wakati akifungua rasmi mkutano wa 67 wa Mawaziri wa Utalii wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism) Kanda ya Afrika (67 CAF) unaoendelea kwenye hoteli ya Radisson Blue jijini Livingstone Zambia.

‘’Mzungumzie mustakabali wa Sekta ya utalii Barani Afrika na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo hasa changamoto ya usafiri wa anga kuwezesha watalii kufika katika maeneo ya utalii na kuweka mikakati ya kukuza na kutangaza  utalii wa Bara la Afrika.’’ Amesema Zurab Pololikashvili

SOMA: Dk Mwinyi awataka mabalozi waibebe nchi

Waziri mwenye dhamana na Utalii wa Zambia, Rodney Sikumba amesema mkutano huo ni fursa pekee kwa nchi za Afrika kuungana katika kushughulikia ipasavyo masuala yanayozuia ukuaji endelevu wa Sekta ya Utalii.

“Kwa muda, tumekuwa tukizungumza juu ya ustahimilivu na ukuaji endelevu wa Sekta ya Utalii kwa sababu ya kile kilichotokea mwaka 2019, wakati huu tunapaswa kuwa na suluhisho bora na sahihi kwa changamoto yoyote inayojitokeza kuzuia uendelevu wa Sekta ya Utalii” amesisitiza.

SOMA: https://maliasili.go.tz/

Pia, amesema inaridhisha kwamba  takwimu za Baraza Kuu la 121 la Baromita ya Utalii Duniani zinaonesha kuwa kwa robo ya kwanza ya mwaka 2024 Watalii wa Kimataifa walifikia asilimia 97% ikilinganishwa na waliofika kabla ya janga la UVIKO – 19 mwaka 2019.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments