MICHANGO ISIZUIE MTOTO KUPATA ELIMU

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Zainab Katimba amesisitiza kuwa uchangiaji katika sekta ya elimu usitumike kumuadhibu mwanafunzi ambaye mzazi wake kashindwa kutoa mchango.

Mhe.Katimba ameyasema hayo leo Julai 26, 2024 akiwa katika ziara ya kukagua miundombinu ya sekta ya elimu katika mamlaka za serikali za mitaa.

Katimba amesema michango yenye kiwango kikubwa inaondoa dhana ya serikali ya elimu bila malipo, hivyo halmashauri zote zinatakiwa kufuata miongozo ya uchangishaji shuleni.

“Nimeona hapa mnautaratibu wa kuchangisha wanafunzi na mmesema mnawachangisha laki sita kwa mwaka, hiki ni kiwango kikubwa, na kimsingi kinaondoa tafsiri ya elimu bila malipo.”

“Huwezi ukamwambia mzazi au ukamwambia mtanzania kwamba elimu bila malipo, anamleta mtoto shule anakutana na mchango mikubwa na sio kila mzazi atakuwa na uwezo wa kutoa."

Kuhusu changamoto ya ukosefu wa kichomea taka na uzio, Mhe.Katimba aliielekeza halmashauri ya Mji Nzega kutumia mapato ya ndani kutatua changamoto hiyo.

Amesema dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha watoto wote wa kitanzania wanapata haki ya kumaliza mzunguko wao wa elimumsingi tena bila malipo.

“Masharti ya michango hii ni kwamba wale wazazi watakaoshindwa kwasababu fulani kutoa michango hii watoto wao wasiadhibiwe kwa kuwambiwa watoto wao wasiingie shuleni. Mchango haimaanishi mtoto akose haki ya kwenda shule kwasababu amekosa mchango wakati amelipiwa ada na Mheshimiwa Dk Samia Suluhu Hassan.

Kuhusu changamoto ya uzio na kichomea taka, Katimba aliiagiza halmashauri ya Nzega kutenga fedha kupitia mapato ya ndani ili kutatua changamoto hiyo.

Naye Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Mji wa Nzega, Lulu Nchiha alisema wazazi wanachangia chakula chenye thamani ya Sh laki sita.








TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments