MJUMBE WA KAMATI YA SIASA CCM (M) SINGIDA CHIFU MGONTO APONGEZA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI IKUNGI

MJUMBE wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Singida,Chief Thomas Mgonto, amepongeza miradi iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru 2024 katika Wilaya ya Ikungi kwamba itaendelea kuleta chachu ya maendeleo katika wilaya hiyo na mkoa mzima kwa ujumla.

Akizungumza leo (Julai 7, 2024) wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru uliotembezwa kwenye miradi saba wilayani Ikungi amesema miradi iliyotembelewa na mwenge huo ambayo ni ya sekta ya afya na elimu hakika itaipaisha wilaya kimaendeleo.

Mgonto amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya jambo la muhimu sana kutoa fedha za ujenzi wa miradi hiyo ambayo kwa asilimia 100 itawanufaisha wananchi.

Amesema wananchi wa wilaya ya Ikungi wamefurahishwa na uwepo wa miradi hiyo ambapo wataendelea kuiunga serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kushiriki katika miradi mbalimbali inayotekelezwa katika wilaya hiyo.

Miradi iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Ikungi ni mradi wa vijana wa ufugaji nyuki na uchakataji asali,Shule ya Sekondari Nkuhi Mtaturu,mradi wa maji kijiji cha Matare na mradi wa nyumba ya watumishi wa hospitali ya wilaya.

Miradi mingine jengo la mama na mtoto Hospitali ya Wilaya ya Ikungi,nyumba za watumishi wa Halmashuri ya Wilaya Ikungi,ukumbi wa halmashuri ya Wilaya ya Ikungi,mradi wa barabara Ikungi-Londoni-Kilimantindi na mradi wa Shule ya Msingi Ikungi.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Thomas Apson amesema Mwenge wa Uhuru 2024 utakimbizwa umbali wa Kilometa 104.2 ambapo miradi 7 yenye  thamani ya Sh. 3,046,807,381.50 iliyopo katika sekta za Elimu, Maji, Afya, Mazingira, Barabara, Ujenzi na Maendeleo ya Jamii imezinduliwa.

Amesema katika fedha hizo zilizotolewa serikali kuu imetoa Sh.bilioni 2.889, wananchi wamechangia nguvu zao Sh.milioni 120,wahisani Sh.milioni 24.486 na halmashuri imetoa Sh.milioni 12.5.













Na Thobias Mwanakatwe,IKUNGI

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments