RABIA: RAIS SAMIA AFUNGUA NCHI, SAUTI MOJA BEI YA KOROSHO

Katibu wa NEC, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndg. Rabia Abdalla Hamid, amesema safari za kikazi nje ya nchi anazozifanya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, zina tija kwa taifa.Amesema hayo leo Julai 28, 2024, katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi, mkoani Mtwara.

Ndg. Rabia amesema, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekuwa akijenga mahusiano mazuri na mataifa mengine, huku akishawishi uwekezaji mkubwa katika sekta mbalimbali nchini, ikiwa ni pamoja na kilimo.

Ameongezea pia kuwa zipo kampuni za nje zikiwemo za Uholanzi, zimewekeza kwenye viwanda vya kubangua korosho na kupandisha kiwango cha ubanguaji kutoka tani 5000 miaka mitatu iliyopita hadi zaidi ya tani 20,000 kwa sasa.

Aidha ametaja kuwa juhudi za Rais za kuunganisha nchi zinazolima korosho Afrika kuwa na sauti moja katika zao hilo, zinalenga kuchochea na kuongeza bei ya korosho kwa manufaa ya wakulima wa zao hilo wakiwemo wa Mtwara.



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments