RAIS SAMIA AMPOKEA MGENI WAKE RAIS WA MSUMBIJI MHE. FILIPE JACINTO NYUSI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Julai, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukiimbwa kwenye mapokezi Rasmi yaliofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Julai, 2024.

Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Julai, 2024.
 

Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Julai, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Julai, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Julai, 2024.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments