WAZIRI MKUU AWASIMAMISHA KAZI WAWILI KILOLO AAGIZA WAFIKISHWE MAHAKAMANI

 

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewamamisha kazi Ofisa Elimu Sekondari wa halmashauri hiyo Nelson Milanzi Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Emanuel Sigachuma ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili kabla ya kufikishwa mahakamani.

Huku aliyekuwa mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ambae sasa amestaafu Laini Kamendu anadawaiwa kushindwa kutekeleza wajibu wake na kusababisha kuwepo kwa mashaka ya matumizi ya zaidi ya Sh Milioni 700 za ujenzi wa bwalo la shule mpya ya sekondari ya wasichana Lugalo wilaya ya Kilolo.

Imeelezwa kuwa pesa hizo Kiasi  ni sehemu ya zaidi ya Sh bilioni tatu zilizotolewa na serikali kupitia mpango wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kujenga katika kila mkoa shule moja ya sekondari ya wasichana ya mkoa na kwa mkoa wa Iringa shule hiyo imejengwa wilaya ya Kilolo.

Awali akisoma  taarifa ya ujenzi wa shule hiyo inayojengwa katika Kata ya Mbigili wilayani Kilolo na ambayo imeanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano mwaka huu, mhandisi wa Halmashauri ya Kilolo alisema ujenzi wa Bwalo hilo ambao umefikia zaidi ya asilimia 40 umegharimu kiasi Cha zaidi ya Sh Milioni 300.

Hata hivyo alipohojiwa  zilipo fedha nyingine za kukamilisha ujenzi wa bwalo hilo, mhandisi huyo alisema zilitumika kukamilisha miundombinu mingine ya shule hiyo, majibu yaliyomkasirisha Waziri Mkuu na kuuliza tena:

“Kwa nini fedha za bwalo zikafanye kazi nyingine tofauti na maelekezo ya serikali yanayoonesha kila jengo linatakiwa kujengwa kwa gharama yake iliyoainishwa."

Akiuliza zilipo zaidi ya Sh Milioni 400 za ujenzi huo, sababu za bwalo hilo kutokamilika na wapi wanafunzi wa shule hiyo wanalia chakula; mhandisi huyo alikaa kimya akionekana hana majibu.

Akimuagiza mwanasheria wa serikali kuhakikisha wawili hao wanafikishwa mahakamani Waziri Mkuu alimtaka Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa kumtafuta popote alipo na kumrejesha Iringa aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Kamendu ili naye aunganishwe katika kesi hiyo.

Aidha Waziri Mkuu amehoji sababu ya halmashauri hiyo kumlipa mkandarasi fedha zake zote pamoja na kwamba hajakamilisha sehemu ya ujenzi wa jengo la utawala, huku akitaka madawati yote katika shule hiyo yaliyotengenezwa chini ya kiwango, yaondolewe mara moja.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments