Zitto ataka uchunguzi huru vitendo vya utekaji

SERIKALI imeshauriwa kufanya uchunguzi huru ili kubaini na kukomesha matukio ya utekaji yanayoendelea nchini.

Zitto ameshauri hivyo leo Julai 2, 2024 kuhusu kuripotiwa tukio la kutoweka mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, Edgar Mwakabela maarufu kama ‘Sativa’ anayedaiwa kutoweka Juni 23, 2024 na kupatikana Juni 27, 2024 katika pori la Hifadhi ya Katavi.

“Uchunguzi huru ufanyike, ili kukomesha matukio haya yaliyoanza kushamiri katika siku za hivi karibuni. Matukio haya yanaharibu taswira ya nchi yetu, yanaturudisha katika zama ambazo wengine tuliamini tumeshatoka,” amesema Zitto.

“Njia pekee ya kukomesha haya ni kufanyika uchunguzi huru na wa kina, ili hatua stahiki zichukuliwe kwa watu watakaohusika na matukio haya,” amesema Zitto na kuongeza kuwa vitendo hivyo vilianza kusahaulika, ila vimeanza kurejea na kuzua hofu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments