Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na Wananchi wa Katoma, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Vijijini, mkoani Kagera, Ijumaa Agosti 9, 2024 wakati akiendelea na ziara yake ya siku sita mkoani humo, waliomsimamisha njiani wakati akitokea Wilaya ya Misenyi, kwenda Bukoba mjini.
Katika ziara hiyo Balozi Dkt. Nchimbi ameambatana na Ndugu Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) - Oganaizesheni, Ndugu Amos Gabriel Makalla, Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo na Ndugu Rabia Abdalla Hamid, Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
0 Comments