NA JOSEA SINKALA, MBEYA.
Wanafunzi wapatao watano waliosoma nchini Nigeria kwa muda wa miaka sita chini ya ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamerejea nchini baada ya kuhitimu kidato cha sita.
Baadaye wanafunzi hao watarudi nchini Nigeria kuendelea na masomo ya elimu ya juu kulingana na matokeo yao yatakavyokuwa.
Wanafunzi waliopokelewa ni Anna Bernard Shitindi, Bernada Emmanuel Fuine, Beauty Japhary, Ayubu Andrew Mwaihola na Suzana Willey Mwakilima wakipokelewa na Meneja wa Tulia Trust Jacqueline Boaz, wazazi na walezi pamoja na walimu.
Meneja wa taasisi ya Tulia trust Jackrine Boazi akizungumza na wanahabari amesema Dkt. Tulia Ackson ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi hiyo isiyo ya kiserikali aliamua kuwasomesha watoto hao ili watimize malengo yao hasa kitaaluma wakiwa wanatokea familia zisizo na uwezo kiuchumi.
Mmoja wa wanafunzi hao Beauty Japhary na Ayubu Andrew Mwaihola mbali ya kumshukuru Dkt Tulia kwa moyo wa upendo wametoa wito kwa wananchi wengine kuiga mfano kwa Dkt. Tulia kusaidia wasiokuwa na uwezo na wasiojiweza.
Kijana Mwaihola anasema "Kuna usemi wa kingereza ambao nikiufafanua kwa kiswahili unasema mshumaa huwa haupotezi mwanga wake kwa kusaidia kuwasha mshumaa mwingine, Dkt. Tulia ni kiongozi ambaye ni mfano mimi nilizaliwa hata simjui baba yangu nikalelewa na mama na kaka na dada zangu lakini Dkt. Tulia Ackson akanichukua na kusema nitafanikiwa na nawahakikishia nitafanikiwa mara mia, Mungu ambariki sana Dkt. Tulia na naomba wa-Tanzania wote mpeni ushirikiano", ameeleza.
Naye Gerard Joseph Emmanuel, kwa niaba ya wazazi na walezi wa watoto hao, amesema familia yake haikuwa na uwezo wa kumsomesha kijana wao hivyo kumshukuru Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson kupitia taasisi yake kwa moyo wake wa upendo na kujali maisha ya wananchi wakiwemo wasiojiweza kiuchumi.
Hafla hiyo fupi pia imehudhuriwa na viongozi wa Vy
Chama cha walimu na shirikisho la walimu watokanao na Chama Cha Mapinduzi ambao wamesema Dkt. Tulia Ackson ni mfano wa kiongozi bora kwani kuwasaidia watoto hao kusoma hadi elimu ya juu wanayoiendea inawapa moyo walimu mara watoto wanapofaulu.
Baada ya mapokezi hayo wanafunzi hao wamepita shule mbili kwa ajili kutoa msaada kwa watoto wenye uhitaji na kuwahimiza kuzingatia masomo kwa faida yao, Taifa na jamii kwa ujumla.
0 Comments