TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewataka viongozi wa vyama vya siasa na mawakala wa vyama hivyo katika Mkoa wa Simiyu kutoingilia zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga pindi litakapoanza kutekelezwa katika mkoa huo.
Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika mkoani humo litafanyika kwa siku saba kuanzia Septemba 04, hadi Septemba 10, 2024 ambapo jumla ya vituo 1,597 mkoa mzima vimeandaliwa kwa ajili ya zoezi hilo.
SOMA: Uboreshaji daftari wapiga kura kuzinduliwa leo
Kauli hiyo imetolewa leo na Makamu Mwenyekiti Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa Mstaafu Mbarouk Salim Mbarouk wakati wa mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoani humo ulifanyika katika ukumbi wa Halmashuari ya Mji wa Bariadi.
Jaji Mbarouk amesema katika zoezi hili, kazi kubwa ya wadau wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa pamoja na makawala wao ni kuhakikisha wanawahasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hili na siyo kuingilia.
SOMA: ‘Nida si lazima uboreshaji daftari wapigakura’
“Napenda kutumia fursa hii kusisitiza kuwa, mawakala au viongozi wa vyama vya siasa hawaruhusiwi kuingilia mchakato wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kituoni,” alisema jaji Mbarouk.
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk leo tarehe 25 Agosti, 2024 amefungua mkutano wa wadau wa Uchaguzi mkoani Simiyu. Kwenye mkutano huo mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwa ni pamoja na mada ya Mkurugenzi wa Uchaguzi pic.twitter.com/d1rd928ADa
— Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (@TumeUchaguziTZ) Augu
0 Comments