TANZANIA MWENYEJI MAONESHO YA 21 YA KAHAWA FEBRUARI 2025

 WAKULIMA na Wafanyabiashara wa Kahawa kutanua Masoko yao kupitia Maonesho ya 21 ya biashara ya Kahawa yaliyoandaliwa na chama cha Kahawa bora za Afrika (AFCA) Kwa Kushirikiana na Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) yanayotarajiwa kufanyika Februari 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na Wanahabari Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa Nchini Primus Kimaryo wakati akitangaza ujio wa Mkutano na Maonesho hayo ikiwa nchi ya Tanzania ndio Muandaaji ,amesema ni wazi ugeni huo utawanufaisha Wakulima,Wafanyabiashara na watu wote wa Sekta ya Kahawa kutokana na kujifunza vitu mbalimbali kutoka nchi shiriki ili kuongeza thamani ya Kahawa inayozalishwa nchini Tanzania.

Hata hivyo Kimaryo ameongeza kuwa ni bahati kwa Maonesho hayo kufanyika kwa mara ya pili ambapo awali yalifanyika 2016 .

"Tanzania ina fursa kubwa katika Maonesho hayo yanadhihirisha ubora wa kipekee wa Kahawa za Afrika na pia yanaimarisha dhamira ya nchi za Afrika katika kukuza Ukuaji na Ushirikiano katika Sekta ya Kahawa Afrika."

Aidha Kimaryo amesema kuonesha namna gani wataweza kupata masoko mapya na kuzitangaza Kahawa zetu mbili zinazolimwa ambazo ni Arabika na Robusta .

Hata hivyo ameongeza kuwa ni wakati wa kuonesha thamani na kupanua masoko na kufikia masoko yaliyokuwa na changamoto.

Kuwepo kwa Maonesho haya ni wazi kuwa nchi imefunguka hivyo fursa kubwa na watu watapata fursa kushiriki hasa wenye Viwanda,Wakulima na wenye migahawa ya Kahawa pia.

Nae Mwenyekiti na Mwakilishi wa Chama cha Kahawa bora za Afrika kutoka Tanzania Amir Hamza ameongeza kuwa Maonesho hayo yanalenga kuwavutia Wawekezaji pamoja na Kutanua Masoko ya Kahawa na Kuipa thamani Kahawa inayozalishwa nchini Tanzania.

Pia amesema Maonesho hayo ya 21 ya Biashara ya Kahawa yatafanyika kuanzia Februari 26 hadi 28,2025 ambapo nchi za Bara la Afrika zitashiriki na kutakuwepo Kongamano ikiongozwa na orodha ya wazungumzaji maarufu kitaifa na Kikanda huku ikiambatana na nafasi ya ,kutoa fursa ya kuonja kahawa,Mashindano ya Watayarishaji Kahawa Afrika na Bidhaa bora zaidi za Kahawa kutoka kote barani bila kusahau watengenezaji wa vifungashio vya Kahawa.
 Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa Nchini Primus Kimaryo akizungumza na Wanahabari Mara baada ya Kutangaza ujio wa Kongamano na Maonesho ya 21 ya Biashara ya Kahawa ambapo nchi ya Tanzania itakuwa Mwenyeji wa Maonesho hayo yanayotarajiwa kufanyika Februari 26  hadi 28,2025 Katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam
 

Mwenyekiti wa Chama cha Kahawa bora za Afrika kwa Upande wa Nchi ya Tanzania   Amir Hamza akizungumza machache na kuwaalika wadau wote wa Sekta ya Kahawa kushiriki katika Kongamano na Maonesho ya 21 ya Biashara ya Kahawa yaliyoandaliwa na chama cha Kahawa bora za Afrika (AFCA) Kwa Kushirikiana na  Bodi ya Kahawa nchini Tanzania (TCB)

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments