MAASAI GLOBAL FESTIVAL 2024 NA TIGO : Agosti 09 & 10 , Watu walifurika katika banda la Tigo kwa nyakati tofauti tofauti pale Eden Garden - Arusha , kujipatia huduma za Kidigitali ikiwemo simu janja aina ya ZTE A34 kwa mkopo , na malipo yake ni Tsh. 650 kwa siku katika Maasai Global Festival 2024 , ambapo Kampuni ya Tigo Tanzania ilishiriki ikiwa na Kampeni yake Kabambe ya " HAKUNA MATATA " kwa ajili ya Watalii.
BURUDANI JUU YA BURUDANI MAASAI GLOBAL FESTIVAL 2024 : Burudani zisizo na kikomo kutoka kwa wasanii Rayvan , Barnaba , Frida Aman , Weusi na wengineo zilitikisa huku Watalii nao wakipata Burudani " HAKUNA MATATA " Kampeni iliyozinduliwa na Tigo yenye lengo la Kuboresha uzoefu wa Watalii na kuhakikisha wanabaki na mawasiliano ya Uhakika na ya haraka wanapozuru vivutio mbalimbali hapa nchini .
Agosti , 09 - 10 Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo Tanzania imeshiriki katika Maasai Global Festival 2024 ikiwa na Kampeni yake Kabambe ya HAKUNA MATATA kwa ajili ya watalii wafikao nchini
" Kampeni ya HAKUNA MATATA inalenga kuboresha uzoefu kwa Watalii , ili kuhakikisha wanabaki na mawasiliano ya uhakika na ya haraka wanapozuru vivutio vyetu vya kitalii , Tunawaletea Vifurushi Maalum vya JAMBO PACKS ambavyo vitawapa watalii huduma bora na rahisi za mawasiliano , watalii wanapotembelea nchi yetu wanahitaji kuwa na mawasiliano bora , si tu kwa ajili ya kujuliana hali na wapendwa wao , bali pia kwa ajili ya kupata taarifa muhimu na kuendesha shughuli zao kwa urahisi " alisema
0 Comments