TANESCO inaendelea na utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme kwenye kisiwa cha chole kilichopo Wilayani Mafia Mkoani Pwani.
Mradi huu unahusisha kuvusha umeme kupitia baharini kwa kutumia waya wa marine cable wenye urefu wa zaidi ya kilomita moja na nusu.
Upatikanaji wa umeme wa uhakika ilikuwa ndoto ya siku nyingi kwa wakazi wa kisiwa cha chole, na utekelezaji wa mradi huu unaenda kubadilisha
Kabisa historia ya muda mrefu ya kisiwa hicho ambacho hakikuwahi kuwa na huduma ya umeme.
Hii ikiwa kati ya juhudi za Serikali chini ya uongozi thabiti wa Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Nishati inayosimamiwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt Doto Biteko kuhakikisha watanzania wote wanapata huduma ya umeme wa uhakika na wa kutosha ili kuchochea shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Chanzo Sayari news
0 Comments