UOGA WA WAANDISHI KUSHINDWA KUFANYIKA HABARI ZA UCHUNGUZI NCHINI

 AMIDI Shule kuu ya uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma, Dkt. Mona Mwakalinga amesema sababu inayopelekea kushindwa kufanyika habari za uchunguzi nchini ni uoga ambao umewakumba waandishi walio wengi.

Amesema uandishi wa uchunguzi ni muhimu kwani unawawajibisha walioko kwenye mamlaka kwani wakienda kinyume habari za uchunguzi zitawamulika,

Ameyasema hayo leo Agosti 30, 2024 katika Kongamano la 14 la Jumuiya ya Wadau wa Habari Afrika Mashariki (EACA) lililoandaliwa na Shule ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC-UDSM) ambalo limewakutanisha watafiti, wanazuoni, wahadhiri, wanafunzi na wataalamu wa sekta ya habari kutoka nchi 25 duniani, lililofanyikia Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

"Waandishi wafanye habari hizi ili waonekane wapo kuisaidia jamii na wenye mamlaka watambue wanatakiwa kufanya kazi zao," amesema

Kwa upande wake Mhadhiri Chuo Kikuu cha Tumaini Dkt Samwilu Mwaffisi amesema aina hiyo ya uandishi inahitaji fedha huku vyombo vingi nchini havina uwezo wa kuwekeza kumwezesha mwandishi afanye kama inavyotakiwa kufanywa.

"Kuna uoga kutokana na matokeo ambayo wengi wanadhani wataingia katika migogoro na wale wanaowachunguza ikiwemo Serikali kwahiyo waandishi wanajipa uoga hata kabla," amesema Dkt. Mwaffisi.

Naye, Mwandishi Nguli nchini Jenerali Ulimwengu amesema kinachopaswa kufanyika ni uwajibikaji kati ya walioko kwenye madaraka ambao vyombo vya habari ndio vyenye jukumu la kuwawajibisha na si kusifia tu waonekane wanafanya kazi.UOGA 


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments