VITONGOJI 3,060 NCHINI KUPELEKEWA UMEME, DKT BITEKO AWATAKA WAKANDARASI KUTOKUWADAI WANANCHI FEDHA ZA ZIADA.

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe Dkt Dotto Biteko amewataka Wakandarasi waliosaini mikataba miradi ya kupeleka umeme kwenye Vitongoji 3,060 na REA akiwa Mtendaji Mkuu kuhakikisha hakuna mwananchi anayedaiwa fedha za zaida katika kufukishiwa umeme kwani serikali Serikali imekwisha kutenga fedha kwaajili ya miradi hiyo.

Dkt Biteko ameyasema hayo Leo hii Agosti 20,2024 Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kusaini mikataba ya miradi ya kupeleka umeme kwenye Vitongoji 3,060 Nchini kwa Vitongoji 15 kila Jimbo.

Na kuongeza kuwa kumekuwa na Taarifa kuwa kuna baadhi ya Wakandarasi wanapoenda kupeleka umeme vijijini wamekuwa wakiomba fedha kwa wananchi ili wawasogezee nguzo za umeme wakati Serikali imeshalipa gharama zote.

"Ziko taarifa za baadhi ya Wakandarasi wetu wanapoenda kupeleka umeme vijijini wanawaomba fedha wananchi kwa hela ambayo Serikali imeshalipa kwamba ili nikusogezee nguzo kwako nipe kiasi hiki. Nataka niwaombe Wakandarasi na REA nikipata taarifa ya mkandarasi yeyote ambaye badala ya kufanya kazi ya kupeleka umeme ameingia katika dili ya kutafuta fedha kidogo kwa Watanzania masikini ambao wao Serikali imejinyima ili kuwapelekea umeme, Mimi sitashughulika na mkandarasi ila nitashughulika na wewe Mtendaji Mkuu REA,kwasababu lazima tufike mahali Watanzania wajue hii ni haki yao kuipata bila watu kutishwa wala kuombwa rushwa".

Aidha Dkt ameleza kuwa Serikali imetenga fedha nyingi ambazo ni zaidi ya bilioni 362 ambazo ni sehemu ya fedha za mapato ya ndani lakini wabia wa maendeleo wanaochangia kwenye mfuko wa Nishati Vijijini hivyo katika Wakandarasi waepuke maelezo na visingizio na badala yake waoneshe matoke ya kazi kwani itakuwa ni aibu pale watakapokuja kufanyiwa tathmini na wadau wa maendeleo ikwemo Bank ya Dunia au Shirika la fedha Duniani wakakuta maelezo badala ya matokeo ya kazi.

"Sasa fedha zilizotengwa na Serikali ni fedha nyingi sana ni zaidi ya bilioni 362,hizi ni fedha fedha ambazo sehemu ya fedha ya fedha hizi tumezipata kutokana na fedha zetu za ndani lakini na wabia wetu wa maendeleo wanaochangia kwenye mfuko wetu wa Nishati Vijijini, Nataka nichukue nafasi hii niwashukuru sana Bank ya Dunia,Serikali ya Norway,Sweden, Umoja wa Ulaya,Shirika la fedha Duniani,Bank ya Maendeleo ya Africa kwa kutoa fedha ya utekelezaji wa miradi hii,itakuwa ni ajabu na aibu kubwa kwa wadau maendeleo wakija kutufanyia tathmini wakute maelezo badala ya miradi kutekelezwa maana kuna watu una.uomba matokeo anakupa maelezo".

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Umeme Vijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy amesema kuwa hadi kufikia Desemba 2024 vijiji vyote vya Tanzania Bara 12,318 vitakuwa vimefikiwa na umeme, hatua ambayo imeongeza hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo ya vijijini.

Na kuongeza kuwa pamoja na mafanikio hayo makubwa ya kupeleka umeme vijijini lakini bado kuna kuna vitongoji takribani 31,532 ikiwa na sawa ya asilimia 49 havijafikiwa na huduma ya umeme.

"Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, naomba kutoa taarifa kuwa hadi kufikia Desemba 2024, vijiji vyote vya Tanzania Bara 12,318 vitakuwa vimefikiwa na huduma ya umeme, hatua ambayo imeongeza hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo ya vijijini".

"Hata hivyo, pamoja na mafanikio makubwa ya kupeleka umeme katika vijiji vyote Nchi nzima, bado takribani vitongoji 31,532 sawa na asilimia 49 havijafikiwa na huduma ya umeme.Mpango wa Serikali kupitia Wakala ni kufikisha umeme kwenye vitongoji 13,000 katika miaka mitatu ijayo, tukianza na vitongoji 3,060 ambavyo mikataba ya utekelezaji wa mradi wa kupeleka umeme katika vitongoji hivyo inasainiwa leo.Hatua hii itafanya asilimia 71 ya vitongoji vyote Nchini kufikiwa na huduma za umeme ifikapo mwaka 2028/29. Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mikataba inayosainiwa leo ni ya mradi wa kupeleka umeme katika vitongoji 3,060 ikiwa ni vitongoji 15 kwa kila Jimbo katika majimbo 204 ya uchaguzi yaliyopo katika mikoa 25 ya Tanzania Bara isipokuwa mkoa wa Dar es salaam.Utekelezaji wa mradi huu utakuwa katika mafungu 25 katika mikoa 25 ya Tanzania Bara, ambapo kutokana na sababu za kimanunuzi mafungu 23 yalipata wakandarasi isipokuwa mikoa ya Singida na Tanga, ambayo zabuni yake itatangazwa tarehe 22 Agosti 2024".

"Mikataba inayosainiwa leo itahusisha ujenzi wa njia za msongo wa kati wa umeme zenye urefu wa km258, ujenzi wa njia za msongo mdogo wa umeme zenye urefu wa km6118, ufungaji transfoma 3,059 pamoja na kuunganisha wateja takribani laki moja (100,000), hatua ambayo itaongeza uunganishwaji wa wananchi na huduma za umeme (connectivity) kwa gharama za takribani Bilioni 360.Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, utekelezaji wa mradi huu utaongeza mtandao wa njia za umeme kwenye vitongoji na hivyo kuwezesha upatikanaji wa umeme kwenye maeneo yenye shughuli za kijamii zikiwemo shule, zahanati na maeneo ya biashara. Hatua hii ya Serikali itachochea maendeleo kwa kupunguza uhamiaji wa watu kutoka vijijini kwenda mijini, matumizi ya vifaa vya kisasa kwenye vituo vya afya, matumizi ya vifaa vya tehama na vya maabara kwenye shule pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo hayo. Utekelezaji wa mradi huu utachochea maendeleo katika vitongoji vilivyolengwa na hivyo kuboresha hali ya uchumi, huduma za jamii na usalama katika maeneo hayo".

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt James Mataragio amesema kuwa wao wataendelea kutunga Sera zenye mwelekeo chanya katika kuhakikisha Taasisi zao ikiwemo REA zinafanikisha malengo ya Serikali hasa lengo la Nishati bora na nafuu kwa Watanzania.

"Hivyo tutaendelea kutunga Sera zenye muelekeo chanya katika kuhakikisha taasisi zetu ikiwemo REA zinafanikisha malengo ya Serikali hasa lengo hili la Nishati bora na nafuu kwa Watanzania".

Mkoa wa Dar es Salaam hautahusika katika miradi hii ya kupeleka umeme katika Vitongoji 3,060 Nchini.





TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments