Watalii wa Brazil Kuanza Kumiminika Tanzania

 Kwa hakika wameshangaa kwa nini hawapo 10 Bora ya nchi zinazoleta watalii kwa wingi na wameshangazwa zaidi na uzuri wa Tanzania; huo ndio mtazamo wa awali kabisa wa kundi la makampuni makubwa ya utalii na vyombo vya habari vya masuala ya safari waliofika nchini leo tayari kuitembelea na kuona uzuri wa Tanzania.

Akizungumza na watendaji wa kampuni hizo takribani 12 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, amesema ujio wa makampuni hayo ambapo waandishi tu waliokuja nao watafikisha habari kwa Wabrazil takribani milioni 85, ni mwendelezo wa visheni ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyefanya filamu ya “Tanzania: The Royal Tour”kuitangaza zaidi nchi yetu.

“Ujio wa wageni hawa ni utekelezaji wa visheni ya Mhe Dkt. Samia Rais wetu na utaona hapa kuna ushirikiano wa Wizara, Bodi ya Utalii na Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Brazil katika kufanikisha hili,” alisema Dr. Abbasi.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Brazil Balozi Profesa Adelardus Kilangi amesema safari hiyo imetokana na ushiriki wa Tanzania wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa WTM ((World Tourism Market) Latin America na moja ya ajenda ilikuwa ni kuitambulisha Tanzania katika soko la utalii la Brazil.

Naye Mratibu wa mawakala hao Bi. Luciana Teixeiana amesema wanafuraha kufika Tanzania na kufurahia mandhari ya jiji zuri la Dar es salaam na wanatumaini watafarijika zaidi na safari yao katika vivutio mbalimbali nchini wakianzia na Serengeti, Ngorongoro na kisha Zanzibar.

Mawakala hao watakuwepo nchini kwa siku 7 na kati yao zipo kampuni mashuhuri za Kibrazil zinazopeleka mamilioni ya watalii nje ya nchi yao ambazo ni kampuni za JACOB Turismo, Golden travel na T4T.

Aidha kwenye kundi hilo wapo wanahabari kutoka televisheni kubwa ya Brazil Globo na mtayarishaji mashuhuri wa kipindi cha “Adrica We Still Don’t Know” Bw. Daniel Steve Sa Silva.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments