KLABU ya Yanga imefanikiwa kunyakua kombe la ngao ya Jamii , mara baada ya kufanikiwa kuichapa Azam Fc fainali kwa mabao 4-1.
Katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam, Azam Fc walianza kupata bao kupitia kwa Feisal Salum “Fei Toto” dakika ya 13 ya mchezo kabla ya Prince Dube kupachika bao la kusawazisha dakika ya 19 ya mchezo.
Yanga SC licha ya kusawazisha bao, waliendelea kulisakama lango la wa pinzani na kufanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa bei wa Azam Fc Yoro Diaby kujifunga akijaribu kuokoa krosi iliyopigwa na beki wa pembeni wa Yanga Chadrack Boka kabla ya Aziz Ki kupachika bao la tatu na kwenda mapumziko matokeo yakiwa Yanga Fc akiwa mbele kwa mabao 3-1.
Kipindi cha pili Azam Fc waliingia uwanjani wakiwa wamefanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji na kuwafanya kuutawala mchezo kwa dakika 20 licha ya kutofika lango la mpinzani mara kwa mara.
Yanga Sc nao walifanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji, ambapo mabadiliko yaliweza kuzaa matunda kwani Mzize ambaye alitokea benchi alifanikiwa kupachika bao la nne akipokea pasi kutoka kwa Chama ambaye nae aliingia kipindi cha pili.
Yanga Sc iliingia fainali baada ya kuichapa Simba Sc 1-0 njsu fainali, huku Azam Fc waliingia baada ya kuichapa Coastal Union kwa mabao 5-2.
0 Comments